Mimi ni Kiongozi mwenye uzoefu mkubwa katika siasa na utumishi wa umma, nikiwa Mbunge wa Jimbo la Ushetu tangu 2021.
Nina rekodi ya mafanikio katika kusimamia na kuratibu miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, afya, maji, barabara na ushirikiano kati ya wananchi na serikali. Pia nimehudumu kwenye ngazi mbalimbali za chama na bunge, nikionyesha uwezo wa kufanya kazi kwa timu, uaminifu, uwajibikaji na ushawishi katika kuleta maendeleo kwa jamii.
i.kufanikisha mchakato wa ununuzi wa pembejeo kwa pamoja katika msimu wa 2020/2021.
i. kuongoza vikao vya Halimashauri ya tumbaku Tanzania na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuongeza uzalishaji wa zao la tumbaku nchini ili kupata bei yenye tija.
ii.. kushiriki katika kusimamia na kuhakikisha watoto walio chini ya miaka 18 hawashiriki katika uzalishaji wa Tumbaku.
iii.kufanikiwa kuyashawishi makampuni ya ununuzi wa tumbaku nchini kuongeza uzalishaji wa zao la tumbaku.
i.kushiriki vikao mbalimbali vya wadau kujadili changamoto na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha zao la Tumbaku nchini, ikiwemo kuongeza utafiti katika upatikanaji wa mbegu bora za tumbaku pamoja na matumizi sahihi ya mbolea.
i.kuanzisha mfuko wa pembejeo kwa Vyama vya Msingi vinavyozalisha zao la tumbaku.
ii.Kufufua kiwanda cha kuchakata Pamba cha KACU Ltd, kilichokuwa kimesimama kufanya kazi kwa miaka ishirini.
iii.kusimamia na kufanikisha mchakato wa uagizaji na usambazaji wa pembejeo za zao la pamba kwa nchi nzima kwa msimu wa 2019/2020 na 2020/2021.
iv.kufanikiwa kulipa malipo ya pili kwa wakulima wa zao la pamba kwa msimu wa 2019/2020.
v.kufanikisha kupungua kwa riba ya Benki katika zao la pamba kutoka asilimia 18% hadi asilimia 2% kwa kutumia L.C (letter of Credit).
i. kuwahamasisha wakulima ambao sio wanachama wa chama cha ushirika kujiunga na chama cha ushirika Mwadui Amcos Ltd.
ii. kusimamia watendaji wa chama cha ushirika cha msingi mwadui kuwa wanaandaa hesabu za chamu na zinakaguliwa kwa wakti kwa kuzingatia sheria ya vyama vya ushirika.
iii. kuhamsisha na kuhakikisha wanachama na wakulima wanaopata huduma chamani kwake wanazingatia njia bora za kilimo cha pamba na tumabaku kwa kusaidiana na maafisa ugani wa eneo husika.
iv. kuhakikisha mwadui Amcos ltd kinakuwa chama cha mfano kwa kushiriki shughuli zote za kiushirika za kimkoa na kitaifa mfano. siku ya Ushirika duniani (SUDI)
i. kushiriki katika mchakato wa ufufuaji wa kiwanda cha kuchakata pamba.
ii. kushiriki katika vikao mbalimbali vya wadau wa Sekta ya Pamba na tumbaku nchini.
iii. kushiriki katika vikao vya kujadili mijengeko ya bei ya pamba na tumbaku nchini.
1. Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya 2021 hadi 2025
2. Mjumbe wa halmashauli kuu ya ccm mkoa wa Shinyanga 2021 hadi 2025
3. Mjumbe wa kamati za kudumu za bunge kilimo Mifugo na maji 2021 hadi 2023
4. Mjumbe kamati ya kudumu ya Bunge maji na mazingira 2023 hadi 2025