
Utaalamu; kwa muda wa miaka kumi na tano nimekua nikifanya kazi ndani ya Serikali pamoja na Jamii na wawekezaji katika kufikia malengo waliojiwekea kupitia shughuli mbalimbali za maisha. Nimekua nikifanya kazi ndani ya Baraza la Mji, nikiitumikia Jamii na wawekezaji kwa miaka kumi na tatu ya ajira, nimepata uzowefu wa kutosha katika masuala ya Uongozi, Utawala na Usimamizi, hii ni taaluma ya kipekee ambayo nimeipata na imejumuika katika ujuzi, sifa na utaalamu wangu wa elimu ambayo imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza umahiri na ufanisi wa kazi zangu. Katika taasisi za Serikali nilianza kujitolea mnamo mwaka 2009, imenichukua kwa kadri ya miaka miwili kama mfanyakazi wa kujitolea ambae nilifanya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi ambayo kwa sasa ni Baraza la Manispaa Magharibi 'B' na nilifanya kazi kama msaidizi wa mambo ya sheria, na hususan katika kitengo cha uhamasishaji na mkusanyaji mapato. Baadae mnamo mwaka 2011, nikawa ni mfanyakazi kazi wa kuajiriwa rasmi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'B' Unguja nikiwa Afisa Sheria wa Halmashauri hiyo na kwa wakati mmoja nikiwa kama mshauri wa masuala ya makusanyo ya mapato. Na kwa kuengezea mimi ni sehemu katika timu ya Uongozi na Msimamizi wa uendeshaji wa maendeleo katika Halmashauri. Kwa msingi huo, naamini kuwa nna ujuzi wa kutosha na uwezo mzuri katika kuweza kufikisha huduma ipasavyo katika kutimiza majukumu yangu ya kazi ikiwaemo kufanya kazi kwa timu na kufanya kazi bila ya msukumo na uelewa katika kutimiza malengo.